ASKOFU MSONGANZILA “AWAASA WAAMINI KUTENGA MOYO WA HURUMA NA KUTENDA MATENDO YA HURUMA”
Written by ReganK on April 8, 2022
Askofu Michael Msonganzila wa jimbo Katoliki Musoma amewaasa waamini kujenga moyo wa huruma na kutenda matendo ya huruma hasa kipindi hiki Cha Kwaresima na hata baada ya Kwaresima kama Yesu alivyokua mwenye huruma hasa kwa wadhambi.
Ameyasema hayo Jumapili ya Tano ya Kwaresima Katika Adhimisho la Misa Takatifu ya baraka na Ufunguzi wa Miradi Mitatu ya Kimkakati Katika Parokia ya Kiabakari Jimbo humo.
Aidha amewaomba waamini kuwa na Tabia ya uchambuzi wa kufuata vyema Sheria kwa lengo la kuokoa uhai wa mwanadamu na Kujua wajibu wetu pia kulinda utakatifu wa ndoa.
Pia amewaomba waamini wasiache kukemea Mila na desturi kandamizi zilizoko ndani ya jamii zetu kwa lengo la kutetea haki ya kila Mmoja wetu.
Naye Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo Meja Jenerali Michael Joseph Isamuhyo amewaomba wananchi kulinda na kutunza Mali zinazojengwa kwani Ni rasilimali nzuri kwa Vizazi vijavyo.
Miradi Hiyo Ni bweni lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 200, Ufugaji na uvunaji wa maji Safi na salama, bafu na vyoo kwa kuzingatia matumizi ya watu wenye ulemavu ( Makundi Maalumu) ambavyo vyote vimejengwa kwa ufadhili wa watu mbali mbali ikiwemo Serikali ya Poland kupitia Mabalozi wake nchini Tanzania.