habari
Katika Kanisa katoliki hakuna ubaguzi kila Mmoja natakiwakufanya kazi yake kadri anavyoweza Ni sehemu ya Mahubiri ya Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Method kilain katika Misa ya Dominika ya Sita ya Pasaka kutoka Kanisa la Bikira Maria Mama Mwenye Huruma Kanisa Kuu Bukoba #RmSautiyaFaraja #Salayashindahofu
Askofu Michael Msonganzila wa jimbo Katoliki Musoma amewaasa waamini kujenga moyo wa huruma na kutenda matendo ya huruma hasa kipindi hiki Cha Kwaresima na hata baada ya Kwaresima kama Yesu alivyokua mwenye huruma hasa kwa wadhambi. Ameyasema hayo Jumapili ya Tano ya Kwaresima Katika Adhimisho la Misa Takatifu ya baraka na Ufunguzi wa Miradi […]
Hii ni homilia iliyotolewa na Padre Maximilian Mutasingwa Paroko msaidizi Parokia ya Rwamishenye Jimbo Katoliki Bukoba wakati wa misa takatifu ya Sikukuu ya kupashwa habari Bikira Maria, misa iliyoambatana na kuwaombea mama wajawazito katika kanisaKuu la Bikira Maria Mama mwenye huruma Kanisa kuu Bukoba. www.radiombiu.co.tz #RmSautiYaFaraja
Ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola katika homilia yake wakati wa Misa takatifu ya Kumshukuru Mungu kwa miaka 50 ya Upadre kwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhshamu Method Kilaini. Misa iliyofanyika katika kanisa kuu la Bukoba Jinbo Katoliki la Bukoba. March 19 2022. www.radiombiu.co.tz
Ni mfululizo wa Mafundisho ya kila Juma kutoka kwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Yohana Paulo II Rwamishenye Jimbo Katoliki la Bukoba Padre Maxmillian Mutasingwa , mafundisho haya hutolewa kila juma katika kanisa kuu la Bukoba Jimbo Katoliki la Bukoba. Karibu ufuatilie sehemu hii ya Mada inayohusu Mfungo wa Kwaresima. www.radiombiu.co.tz #RmSautiYaFaraja
Na Patrick P. Tibanga Radio Mbiu. Waamini wakatoliki wamehimizwa kumpenda na kumwamini mama Bikira Maria na kukimbilia ulinzi wake pamoja na kuvichangia na kuviwezesha vyombo vya kanisa. Hayo yamesemwa na Padre Adeodatus Rwehumbiza Paroko wa Parokia ya Bukoba, katika kilele cha hija ya Bikira Maria wa Lurdi, Nyakijoga Parokiani Mugana , Misa iliyoongozwa na Askofu […]
Leo tutafakari tendo la kwanza la uchungu ambalo ni Yesu anatoka jasho la damu. Kadiri ya Injili, baada ya Yesu kuweka Ekaristi Takatifu kwenye karamu ya mwisho, alikwenda kuanza rasmi mateso yake katika bustani ya Getsemani. Dhambi iliingia katika bustani ya Eden na mateso yatakayoondoa dhambi yanaanza katika bustani ya Getsemani. Yesu alionekana […]
Ni Padre Athanasius Mutasingwa Padre wa Jimbo Katoliki la Bukoba katika neno la Shukrani kwenye Misa ya jubilei ya Miaka 25 ya Utume wa Upadre. www.radiombiu.co.tz #RmSautiYaFaraja
Ni mafundisho ya kila juma yanayotolewa na Paroko wa Parokia ya Minziro Jimbo Katoliki la Bukoba Pade Dkt Faustine Kamugisha, Mafundisho haya hutolewa kila Alhamis saa 11 jioni katika Kanisa kuu la Bukoba, Juma hili mada ilikuwa ni Neema ni Mtego. wote mnakaribishwa kuhudhuria mafundisho haya katika Kanisa kuu. www.radiombiu.co.tz #RmSautiYaFaraja
Mtakatifu John Paul II, alizaliwa mwaka 1920 Mei 18, huko Wadowice Poland. Akabatizwa na kuitwa Karol Józef Wojtyła. Alisoma katika mji wa Kraków , katika chuo kikuu cha Jagiellonian ,na baadae akajiunga na seminari ya Clandestine iliyokuwa chini ya Askofu wa Krakow. Na tarehe 1 Novemba 1946, alipata daraja la Upadri. Tarehe 28 September 1958 […]