Kanisa
Page: 2
Papa Yohane Paulo wa pili, ni mtakatifu wa nyakati zetu, aliyechaguliwa kuwa papa tarehe 16/10/1978 na akaanza rasmi upapa tarehe 22/10/1978 akiwa ni papa wa kwanza kutoka Poland na wa papa 264. Mt. Yohane Paulo II, ambaye aliitwa Karol Josef Wojtyla, alizaliwa tarehe 18/5/1920 huko Wadowice Poland wakati wa utawala wa Wanazi. Alisoma seminari ya […]
Sava alizaliwa katika familia ya kifalme mwaka 1174 akiwa mtoto wa tatu kiume wa Stefano wa kwanza, mfalme wa Serbia huko Yugoslavia. Alipata malezi na elimu bora kama mwana wa mfalme. Alipokuwa na umri wa miaka 17 alijiunga na wamonaki wa Mlima Athos huko Ugiriki. Baada ya miaka 4 utawani, baba yake mzazi alijiuzulu ufalme […]
Mama Kanisa anamkumbuka leo Stefano Shemasi na Shahidi wa kwanza katika ukristo. Siku ya Mt. Stefano inafuata tu mara baada ya kusherehekea kuzaliwa Mkombozi, ili kutukumbusha nasi kuyatoa maisha yetu bila kujibakiza kwa Mtoto Yesu. Kadiri ya Kitabu cha Matendo ya Mitume, Stefano ni mmoja wa wale mashemasi saba waliochaguliwa na Mitume kusaidia kufanya huduma […]
Mwenyeheri alizaliwa huko Italia mwaka 1592 katika familia ya wacha Mungu. alionekana mwenye akili nyingi na ibada kwa Bikira Maria wa Loreto aliyoirithi kutoka kwa Baba yake aliyefariki Antony akiwa na miaka 10. Akiwa na miaka 17, Antony alijiunga na shirika la Wa-Oratori alilolianzisha mt. Filipo Neri. Kama mwanafunzi, Antony alionesha uwezo mkubwa katika masomo […]
Tunamkumbuka Mtakatifu Lucia -bikira na mfiadini. Lucia alizaliwa mwaka 283 katika familia yenye hadhi na ya kitajiri. Baba yake alifariki wakati Lucia akiwa na umri wa miaka 5 akimuacha katika malezi ya mama ambaye alimlea katika imani thabiti ya kikatoliki, lakini hakuwa na ulinzi kamili kwani alikuwa na asili ya kigiriki. Masimulizi yanaeleza kuwa Lucia […]
Leo Kanisa linamkumbuka na kumuenzi Mt. Yohana Francisca wa Shantal, Mtawa na Mwanzilishi wa shirika. Francisca alizaliwa Januari 28 1572 katika familia ya kawaida isiyo na umaarufu wowote huko Dijon Ufaransa. Mama yake alifariki Francisca akiwa na miezi 18 tu, hivyo alilelewa katika maadili mazuri na imani ya kikatoliki na baba akisaidiana na ndugu zake. […]
Kanisa linamkumbuka na kumuenzi Mt. Damas wa kwanza – Papa, askofu wa Roma aliyezaliwa mwaka 305 katika familia yenye uchaji huko Hispania. Yeye pamoja na wenzake walirudi Roma ambako alipadrishwa na mwaka 366 wakati wa matatizo mengi sana aliteuliwa kuwa Papa. Mt. Damas aliitetea imani kwa nguvu zake zote, ndiyo maana aliitisha mikutano mingi kuwapinga […]
Olimpia alizaliwa katika familia ya kitajiri. Wazazi wake walifariki akiwa bado mdogo sana hivyo alilelewa na mwanamke mwadilifu na mwenye busara, aliye mfundisha sala na maadili bora. Olimpia alikuwa binti mzuri sana na tabia njema. Mt. Gregori wa Nazienzi anamueleza kama “kielelezo cha wema”. Aliolewa na kijana mwenye tabia ngumu ambaye aliyefariki ndani ya majuma […]