Kanisa

Page: 3

Mama Kanisa anamkumbuka leo Mt. Ambrose Askofu na Mwalimu wa Kanisa, mtoto wa gavana wa Ufaransa. Ambrose alizaliwa huko Tria Ujerumani mwaka 340 katika familia ya Waroma. Tangu utoto wake alikuwa mwema na mpenda watu. Akiwa mtoto mdogo, aliwasingikiza mama na dada yake kanisani, ambako aliwaona wakibusu pete ya askofu, kwa utani akawaambia “ubusuni mkono […]

Mtakatifu Klementi tunayemwadhimisha leo, aliongokea  imani ya kweli kwa uongozi wa Mt. Petro. Katika barua zake Mt. Paulo anamtaja kama mwenzi wa masumbuko yake ambaye jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima wa milele (Fil. 4:3). Klementi ni papa wa tatu baada ya Petro na alilitawala Kanisa kwa utaratibu na nguvu tangu mwaka 88 hadi […]

Caecilia ni shahidi maarufu wa Roma, aliyeyatolea maisha yake kumtumikia MUNGU. Caecilia alipenda sana kuimba sifa za Mungu. Tangu utoto wake, alitamani kujitoa kwa ajili ya Kristo. Masimulizi yanatuambia kuwa Caecila aliolewa na mpagani  Valerian. Wakati wa usiku wakiwa na Valerian, Caecilia alimwambia mumewe ,” Nina siri kubwa sharti nikuambue:karibu yangu husimama malaika mkuu anayenilinda, […]

Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya kutolewa Bikira Maria hekaluni. Masimulizi ya kale, yanadhihirisha kwamba wazazi wake Yoakimu na Anna walimtolea mwana wao kwa Mungu katika hekalu huko Jerusalem. Tunapofanya sikukuu hii, tunamtukuza na kumshukuru Mungu ambaye alimchagua Bikira Maria awe Mama wa Mungu. Heshima ile kubwa na ya ajabu ambayo Mungu alimpa Bikira Maria kwa […]

 Mt. Andrea alizaliwa  mwaka 1521 huko Napoli huko Italia akaitwa Lanseloti. Alipopewa upadre, kwanza alisomea sheria na alipohitimu alipewa kazi ya wakili katika baraza la Kanisa. Katika kutekeleza wajibu huu, Lanseloti alisema uongo kidogo. Alipofikiri moyoni alitubu tangu hapo, aliondoka barazani asitake zaidi kuiponza roho yake na akaingia katika jamaa ya Wateatini. Akiwa utawani, alipata […]

Mtakatifu Hilda alizaliwa huko Uingireza mnamo mwaka 614 katika familia ya Kifalme. Alibatizwa akiwa na umri wa miaka 13 wakati wa Pasaka Aprili 12 627. Hilda aliamua kuishi maisha ya kikristo yaliyo jawa fadhila nyingi. Akiwa na miaka 33, alijiunga na monasteri. Akiwa utawani, Hilda alizidi kukua katika fadhila njema hasa ya uongozi. Kama mkuu […]

      Mama Kanisa leo anaadhimisha kutabarukiwa makanisa ya watakatifu Petro na Paulo kwa sababu ya kuwaenzi hawa walio miamba ya imani Katoliki. Basilika la Mt. Petro lilijengwa juu ya kaburi la Petro Mtume kwenye kilima cha vatikano Roma wakati wa utawala wa Papa Silvesta I. Baada ya muda mrefu, lilijengwa kanisa jipya na kubwa […]

KUMBUKUMBU YA KUPEWA DARAJA TAKATIFU YA UASKOFU, KUSIMIKWA KUWA ASKOFU WA JIMBO NA KUZINDULIWA JIMBO KATOLIKI LA KAYANGA. Leo Jumanne 06/11/2018 ni Kumbukumbu ya Miaka 10 ya Kuzinduliwa Jimbo Katoliki la Kayanga, Kupewa Daraja Takatifu ya Uaskofu na Kusimikwa Kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga Kwa Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, Askofu wa Jimbo Katoliki […]

Kanisa linamkumbuka leo  Yohane Paulo wa Pili- Papa na mtakatifu wa zama zetu hizi. Alizaliwa huko Wadowice Poland 18/5/1920 wakati wa utawala wa ki Nazi na kupewa jina la Karol Josef Wojtyla. Alipata kazi katika kiwanda cha kemikali mwaka 1940. Akiwa na miaka 20, alifiwa na wazazi wake pamoja na ndugu yake. Katika huzuni na […]

 Wamiliki, watangazaji na watumiaji wa vyombo mbalimbali vya habari vya Kanisa wameaswa kushiriki katika uinjilishaji na kutumia dominika ya misioni katika kuendeleza utume wa Kanisa, malezi sambamba na ukuzaji imani. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Mashirika ya Uinjilisha kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (T.E. C) Padre DAKTARI JOVITUS MWIJAGE wakati akitoa […]


Current track

Title

Artist