katekesi

Ni mafundisho ya kila juma yanayotolewa na Paroko wa Parokia ya Minziro Jimbo Katoliki la Bukoba Pade Dkt Faustine Kamugisha, Mafundisho haya hutolewa kila Alhamis saa 11 jioni katika Kanisa kuu la Bukoba, Juma hili mada ilikuwa ni Neema ni Mtego. wote mnakaribishwa kuhudhuria mafundisho haya katika Kanisa kuu. www.radiombiu.co.tz #RmSautiYaFaraja

WAFAHAMU MATUMIZI YA MAJI..!? Wakristu wa kwanza walijuamatumzi ya maji kwasababu ya hali zake njema. Tertulliano anawakumbusha wakristo wengine kwamba hata kama walitoka bafuni kabla ya Sala,waendapo kusali budi wanawe mikono yao {De.Orat.C 13} Klementi wa Alexandria anaongea juu ya kunawa mikono kabla ya maombi kama alama ya usafi wa ndani {Stromat.iv,22} Padre anatazamiwa kuosha […]

Mtakatifu Yasinta alizaliwa mwaka 1585 tarehe 16 Machi katika familia ya kitajiri ya Marcantio na Ottavia. Kutokana na uwezo mkubwa wa familia, Yasintha alipatiwa elimu bora. Akiwa na miaka 20 alichumbiwa na kijana toka familia tajiri. Akiwa katika maandalizi ya ndoa yao,  alikataliwa na badala yake mdogo wake akaolewa. Kitendo hiki kilimuhuzunisha sana. Baada ya […]

Mt. Anthony alizaliwa tarehe 23 /12/ 1807 Sallent karibu na Barcelona huko Hispania. Baba yake alikuwa mshona nguo na mfanyabiashara. Athony alifanya biashara hii  na kwa muda wake wa ziada alijifunza kilatini na uchapaji. Mwaka 1827, alianza malezi ya upadre na alipewa daraja ya upadre mwezi Juni 13,1835 katika sherehe ya Mt. Anthony wa Padua. […]

Mt. Yohane Capistrano alizaliwa tarehe 24/6/1386 katika utawala wa Naples. Kwa moyo wake wa kishujaa na kuupenda ufalme, Mfalme Ladislaus alimchaguliwa kuwa gavana wa Perugia. Kwa kiu ya kumtumikia mfalme wa kweli, alijiunga na Maisha ya utawa wa Mt. Francis baada ya kuamua kumtumikia Kristo, Mfalme wa Milele. Aliiacha kazi yake na kuachana na binti […]

Papa Yohane Paulo wa pili, ni mtakatifu wa nyakati zetu, aliyechaguliwa kuwa papa tarehe 16/10/1978 na akaanza rasmi upapa tarehe 22/10/1978 akiwa ni papa wa kwanza kutoka Poland na wa papa 264. Mt. Yohane Paulo II, ambaye aliitwa Karol Josef Wojtyla, alizaliwa tarehe 18/5/1920 huko Wadowice Poland wakati wa utawala wa Wanazi. Alisoma seminari ya […]

Mt. Teresa wa Avila alizaliwa Hispania tarehe 28/3/1515 na Baba Alonso Sanchez na mama Beatrix. Walimlea katika maadili  mema. Akiwa bado mdogo Teresa na kaka yake Rodrig walitoroka kwenda kuyatolea maisha yako kama mashahidi  wakati wa madhulumu ya Moors. Teresa alijiunga na utawa akiwa na miaka 15, ambako aliishi kitakatifu akijita katika sala na maonano […]

Mt.Margaret   Alakoki alizaliwa Julai 22 1647 katika ufalme wa Ufaransa. Akiwa bado aliugua sana homa kali iliyomfanya abaki amelala kwa miaka 4. Kwa muda wote huu, alisali na kuweka ahadi kwamba akipona ataishi maisha ya ufukara katika utawa. Kwa maombezi ya Mama Maria alipona, ndipo alipoongeza jina Maria katika majina yake. Margaret aliisahau ile […]

Mt. Seraphin alizaliwa huko Italia mwaka 1540 katika familia ya kimaskini ya Jerome De Nicola na Theodora. Wazazi hawa walimlea katika maadili bora akiwa na jina Felix. kwasababu ya hali ya familia yake, Felix alifanya kazi ya kuchunga mifugo. akiwa na miaka 16, alijiunga na wakapuchin na kupewa jina Seraphin alipoweka nadhiri. Akiwa utawani, Seraphin […]

Papa Yohane XXIII alizaliwa  tarehe 25 Novemba 1881 huko Italia akiwa ni mtoto wa nne  kati ya watoto 14 wa familia ya wakulima  ya Giovanni Battista Roncali na Marianna Giulia Mazzolla. Jina lake la asili ni Angelo Giusseppe Roncali.  Alipewa daraja ya Upadre tarehe 10/8/1904. Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, Padre Roncali alihudumu […]


Current track

Title

Artist