habari
Page: 5
Leo ni maadhimisho ya miaka 57 tangu Tanganyika (Tanzania Bara) ipate uhuru wake kutoka kwa ukoloni wa Uingereza, kabla ya kuwa chini ya Uingereza Tanganyika iliwahi kuwa chini ya Ujerumani mpaka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Tanganyika ni jina la kihistoria la sehemu kubwa ya Tanzania ya leo, yaani ile yote isiyo […]
Kanisa leo linaadhimisha kuzaliwa kwake Bikira Maria aliyezaliwa bila dhambi ya asili. Ni sherehe ya Maria Imakulata, yaani, yeye asiye na doa wala dhambi. Mama Maria alikingiwa dhambi ya asili kwa mastahili tarajiwa(anticipated merits of Jesus’ death) kifo cha Kristo.Kwa Mungu yote yanawezekana Mk. 10:27, hivyo Yeye aliye mtakatifu lazima aishi katika utakatifu, ndiyo maana […]
Mama Kanisa anamkumbuka leo Mt. Ambrose Askofu na Mwalimu wa Kanisa, mtoto wa gavana wa Ufaransa. Ambrose alizaliwa huko Tria Ujerumani mwaka 340 katika familia ya Waroma. Tangu utoto wake alikuwa mwema na mpenda watu. Akiwa mtoto mdogo, aliwasingikiza mama na dada yake kanisani, ambako aliwaona wakibusu pete ya askofu, kwa utani akawaambia “ubusuni mkono […]
KUMBUKUMBU YA KUZALIWA Leo Jumanne 04/12/2018 ni Kumbukumbu ya Miaka 51 ya Kuzaliwa Mhashamu Flavian Matindi Kassala, Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Askofu Flavian Matindi Kassala Alizaliwa 04/12/1967 Huko Sumve, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza. Askofu Flavian Matindi Kassala Alipewa Daraja Takatifu ya […]
Wajuzi wa mambo husema kuwa tone hujaza Ndoo naaaam kwa kuangalia sehemu ya video hii unaweza kupata maana halisi ya msemo huu. Senene ni moja wapo ya biashara kubwa katika ukanda huu wa ziwa hasa mkoa wa Kagera na maeneo jirani na hata nchi jirani kama Uganda ambapo huko hufahamika zaidi kama Ensenene, ni moja […]
Mtakatifu Klementi tunayemwadhimisha leo, aliongokea imani ya kweli kwa uongozi wa Mt. Petro. Katika barua zake Mt. Paulo anamtaja kama mwenzi wa masumbuko yake ambaye jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima wa milele (Fil. 4:3). Klementi ni papa wa tatu baada ya Petro na alilitawala Kanisa kwa utaratibu na nguvu tangu mwaka 88 hadi […]
Caecilia ni shahidi maarufu wa Roma, aliyeyatolea maisha yake kumtumikia MUNGU. Caecilia alipenda sana kuimba sifa za Mungu. Tangu utoto wake, alitamani kujitoa kwa ajili ya Kristo. Masimulizi yanatuambia kuwa Caecila aliolewa na mpagani Valerian. Wakati wa usiku wakiwa na Valerian, Caecilia alimwambia mumewe ,” Nina siri kubwa sharti nikuambue:karibu yangu husimama malaika mkuu anayenilinda, […]
Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya kutolewa Bikira Maria hekaluni. Masimulizi ya kale, yanadhihirisha kwamba wazazi wake Yoakimu na Anna walimtolea mwana wao kwa Mungu katika hekalu huko Jerusalem. Tunapofanya sikukuu hii, tunamtukuza na kumshukuru Mungu ambaye alimchagua Bikira Maria awe Mama wa Mungu. Heshima ile kubwa na ya ajabu ambayo Mungu alimpa Bikira Maria kwa […]