Kanisa Katoliki ni jina linalotumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya Papa wa Roma kama mkuu wa urika wa Ma askofu juu yake lote.
Ndilo kubwa kabisa kati ya
madhehebu yote ya dini hiyo, likikusanya nusu ya wafuasi wote wa Yesu.
Hata hivyo, Wakristo wa madhehebu mengine wanaokubali kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli wanatafsiri tofauti sehemu inayokiri Kanisa la kweli kutambulishwa na sifa nne , ya tatu ikiwa kwamba ni katoliki : “Tunasadiki Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume”.
Kanisa Katoliki, likiwa na miaka karibu elfu mbili, ni kati ya miundo ya zamani zaidi iliyopo duniani na imechangia kwa kiasi kikubwa ustaarabu wa Magharibi , ingawa baada ya mwisho wa Karne za Kati athari yake inazidi kupungua, ilivyo wazi hasa katika masuala yanayohusu jinsia na uzazi.
Imani ya Kanisa hilo inatokana na
ufunuo wa Mungu ulivyotolewa kwa
Israeli na ulivyokamilishwa na Yesu ambaye alimtambulisha kama Baba na alilianzisha kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa juu ya Mitume wake.
Ni imani inayoungamwa katika ubatizo ,
sakramenti ya kwanza na mlango wa sakramenti nyingine sita: kwamba Mungu ni mmoja tu katika nafsi tatu:
Baba , Mwana na Roho Mtakatifu .
Imani hiyo inatakiwa kutekelezwa katika maadili maalumu yanayotegemea upendo ambao ndio kuu na uhai wa mengine yote.
Kutokana na juhudi za kutekeleza
matendo ya huruma kwa yeyote mwenye shida, Kanisa Katoliki anatoa huduma za elimu na afya kuliko taasisi nyingine yoyote duniani kote.
Kama kielelezo cha utakatifu ambao waamini wote wanaitiwa, Kanisa linapendekeza watu wa Agano la Kale na wa Agano Jipya , hasa Bikira Maria , lakini pia wale waliojitokeza zaidi katika historia yake kama watakatifu.
Baadhi yao wana wafuasi wengi wanaounda familia za kiroho, mara nyingi kama mashirika ya kitawa yenye karama mbalimbali.
Maana ya jina
Neno “katoliki” linatokana na kivumishi cha Kigiriki καθολικός (katholikòs ), lenye maana ya «kamili, kadiri ya utimilifu», kinyume cha «vipandevipande».
Tunalikuta kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wa Smirna mwanzoni mwa
karne II : «Alipo Yesu Kristo ndipo lilipo Kanisa Katoliki»
Ndivyo alivyolitofautisha na makundi madogomadogo yaliyokuwa yameanza kujitenga nalo.
Imani yake kuhusu fumbo lake kama ushirika Kanisa hilo linaamini kuwa ndani yake linadumu moja kwa moja Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu Kristo ambalo wanaunganishwa nalo wote wanaobatizwa katika madhehebu yoyote.
Tofauti kati yao ni kwamba baadhi (Wakatoliki) wana ushirika kamili nalo, wakati wengine (hasa Waorthodoksi,Waorthodoksi wa Mashariki na Waprotestanti ) wana ushirika nalo kwa viwango mbalimbali, kadiri wanavyokubali mafundisho, sakramenti na uongozi wake.
Hatimaye, Kanisa hilo linaamini kuwa wale wote wasiobatizwa wanaitwa naMungu kufanya hivyo na kujiunga nalo ili wafikie wokovu ulioletwa na Yesu Kristo.
Kati ya madhehebu ya Kikristo, Kanisa Katoliki linakusanya waamini 1,254,000,000, yaani nusu ya wafuasi wote wa Yesu , na 17.7 % ya binadamu wote, likiwa na asilimia kubwa ya waamini kati ya wananchi wa Amerika na Ulaya.
Hata hivyo Wakatoliki kwa muda mrefu sasa wanaongezeka hasa katika ma bara ya Afrika na Asia.
www.radiombiu.co.tz
#rmsautiyafaraja