NENO LA MKURUGENZI WA HABARI RADIO MBIU.

UTANGULIZI:

Mpenzi mdau wa Radio Mbiu – Sauti ya Faraja, ningependa kutumia nafasi kwanza kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha, kwa namna moja au nyingine, kuanzisha kituo hiki cha Radio Mbiu.  Pili kukushukuru wewe mdau wetu kwa kuwa pamoja nasi kuanzia mwanzo wa radio hii.

Pia nitumie nafasi hii kukukaribisha rasmi katika kazi hii njema ya kueneza Habari Njema kwa watu wote.  Ofsi zetu za Radio Mbiu zipo maeneo ya Bunena, Manispaa ya Bukoba katika mkoa wa Kagera – Tanzania. Tunapatikana kupitia masafa ya 104.9 FM na tumeenea zaidi katika wilaya za Manispaa ya Bukoba, Bukoba Vijijini, Misenyi, Muleba, Karagwe na baadhi ya sehemu za Biharamulo, Ngara na Kyerwa.  

Radio Mbiu yenye kauli mbiu yake ‘Sauti ya Faraja’ inawalengwa watu wa kila nafasi na rika.  Inawalenga watoto kwa kupitia vipindi mbalimbali hasa kile cha watoto kinachorushwa kila siku ya Jumamosi saa 3.00 asubuhi.  Walengwa wengine ni vijana, wtu wa rika la kati na wazee. Radio Mbiu ni faraja kwa wagonjwa, wazee, wenye mahangaiko mbalimbali za maisha na watu wote.  Aina ya vipindi virushwavyo na Radio Mbiu ni pamoja na vipindi vya maadili, Maandiko Matakatifu, Katekisimu Katoliki, vipindi vya afya, lishe, sheria, usalama barabarani, taarifa ya habari, michezo na burudani za nyimbo mbalimbali kwa rika zote.

MALENGO

Kuhabarisha, kuelimisha, kushirikisha, kuburudisha

Kukupa faraja, Radio Mbiu ni rafiki yako wa kukupa faraja wakati wa uhitaji, wakati wa huzuni, wakati wa magumu, wakati wa furaha, ukiwa safarini, ukiwa kazini, ukiwa nyumbani, ukiwa kwenye shughuli zako, ukiwa shambani na mahali popote.

Kukujenga kimaadili kupitia vipindi vyake mbalimbali kwa watoto, vijana, wazee, wake kwa waume na rika zote kwa wakati wote.

Kukuletea matumaini mapya kupitia Habari Njema

MATARAJIO

Ni matarajio yangu kuwa wewe mdau wa Radio Mbiu;

Utaipokea, kuipenda na kuisikiliza.

Utawahamasisha wengine kuisiskiliza

Kuwafikia watu wengi ndani ya Bukoba, Kagera, Tanzania na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Kuwapa ‘vitu’ vilivyo bora kabisa kupitia waandaaji mbalimbali waliobobea kwa kuwaandalia vipindi vilivyo bora sana.

Utapata kitu tofauti na ulivyozoea kupata kwenye radio zingine.  Hii inatokana na dhamira ya dhati ya timu ya watumishi wa Radio Mbiu kukufanya ujitambue na kujisikia tofauti unayestahili kupata kitu tofauti na bora.

MWALIKO

Ninatumia fursa hii kukualika wewe mdau wa Radio Mbiu – Sauti ya Faraja kupenda kuisikiliza Radio Mbiu kila wakati na kila mahali.  Pia nunakualika uiunge mkono kwa kuwahamasisha wengine waisikilize, waikubali na kwa pamoja kuimiliki Radio hii kuwa mali yako.

HITIMISHO

Kwa kuhitimisha, niendelee kukushukuru wewe mdau na kukuomba uendelee kuipenda, kuisikiliza na kuiunga mkono Radio yako ili kuweza kufikia malengo yake na malengo yako ya maisha ya kiroho na kimwili.  Kwa kupitia watalaam wetu, tunaahidi kukuandalia vipindi bora na mada motomoto zitakazokufanya uhabarike na kushiriki kuwahabarisha wengine. Karibu tuwe sote siku zote kwani wewe ndiwe sababu ya kuwepo na kufanukiwa kwetu.

 

Radio Mbiu – Sauti ya Faraja.

Ni mimi mtumishi wenu,

Pd. Deodatus Kagashe Katunzi

Mkurugenzi wa Idara ya Matangazo.

 


Current track

Title

Artist

Pakua programu ya simu ya Apple
Send this to a friend