Mtakatifu John Paul II, Papa Oktoba 22

Written by on October 22, 2021

Mtakatifu John Paul II, alizaliwa mwaka 1920 Mei 18, huko Wadowice Poland. Akabatizwa na kuitwa Karol Józef Wojtyła. Alisoma katika mji wa Kraków , katika chuo kikuu cha Jagiellonian ,na baadae akajiunga na seminari ya Clandestine iliyokuwa chini ya Askofu wa Krakow. Na tarehe 1 Novemba 1946, alipata daraja la Upadri. Tarehe 28 September 1958 alipata daraja la Uaskofu na tarehe 26 Juni 1967 akawa kardinali. Mwaka 1978 October 16 akachaguliwa kuwa Papa. Hapo akachukua jina la John Paul II, Akasafiri nchi 129, akatangaza wenye heri 1,340 , akatangaza pia Watakatifu 483. Papa John Paul II, alikufa tarehe 2 April 2005, huko Vatican. Akatangazwa mwenyeheri tarehe 1 Mei 2011 na Papa Benedict XVI. Tarehe 27 April 2014, alitangazwa Mtakatifu na Papa Francis
 
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Abercius Marcellus Wt. Alexander, Heraclins, na wenzao M/h. Alix Le Clercq Mt. Alodia Mt. Benedict wa Macerac Mt. Bertharius Mt. Donatus wa Fiesole Mt. Mark Mt. Mary Salome Mt. Mellon Mt. Moderan Mt. Nepotian Mt. Nunctus Mt. Philip Mt. Philip wa Heraclea Mt. Verecundus Mtakatifu John Paul II, Wenye heri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee.
www.radiombiu.co.tz
#RmSautiYaFaraja

Current track

Title

Artist

Pakua programu ya simu ya Apple
Send this to a friend