Radio Yetu

HISTORIA YA RADIO MBIU

RADIO MBIU ni radio changa lakini yenye historia inayotufanya turudi nyuma kama miaka nne hivi.  Radio Mbiu ni zao la pamoja kati ya Marafiki wa Radio Maria Tanzania na Jimbo la Bukoba. Ni radio ambayo inamilikiwa na AMANI BROADCASTING LIMITED ambayo ilisajiliwa na Brela tarehe 01/04/2014. Amani Broadcasting Limited ikachukua jukumu la kuanzisha Radio Mbiu na tarehe 07/07/2014 Radio Mbiu ilisajiliwa rasmi kama radio ya kibiashara na kuweka ofisi zake katika eneo la Bunena katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Radio Mbiu ilipata kibali cha kujenga kituo cha radio (construction permit CP) kutoka TCRA tarehe 01/09/2016 chenye namba CP. No. BA 149/358/012/31 na kupatiwa masafa ya kwanza 88.9 fm ambayo badaye yalibadilishiwa kutokana na ukweli kwamba masafa hayo tayari yalikwisha pewa radio nyingine. Hivyo masafa yakabadilishwa na kuwa 104.9 fm. Tarehe 13/04/2018 ilikaguliwa na TCRA na kuruhusiwa kuanza majaribio ya mwezi mmoja ambacho kipindi hicho kilimalizika tarehe 12/05/2018. Tarehe 13/05/2018 Radio Mbiu yenye kauli mbiu ‘SAUTI YA FARAJA’ iliruhusiwa rasmi kuanza kwa vipindi. Radio Mbiu imepatiwa leseni ya hadhi ya Wilaya (District License) ambayo kwa mujibu wa sheria mpya ya TCRA inaruhusiwa kuwa na masafa matatu yaani hayo 104.9 fm ambayo ni kwa ajili ya mkoa wa Kagera na mengine mawili zaidi ambayo inaweza kufungwa katika mikoa mingine yoyote miwili. Masafa hayo yanatakiwa yatumike ndani ya mwaka mmoja tangu kupata leseni. Uongozi wa radio utaamua radio itajitanua kuelekea mikoa gani baada ya Kagera. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa mikoa inayopakana na mkoa wa Kagera. Mingine itafuata baada ya kubadilisha hadhi ya leseni kutoka ya Wilaya na kwenda ya Mkoa (Regional License).

Pamoja na kuruhusu kuanza kwa vipindi tangia tarehe 13/05/2018 lakini uzinduzi rasmi wa watangazo yalianza tarehe 29/05/2018. Karibu tupate faraja ya Neno la Mungu, tafakari na mengine mengi yatakayokujenga kiroho na kimwili.

 


Current track

Title

Artist

Pakua programu ya simu ya Apple
Send this to a friend