Na Patrick P. Tibanga
Radio Mbiu.
Waamini wakatoliki wamehimizwa kumpenda na kumwamini mama Bikira Maria na kukimbilia ulinzi wake pamoja na kuvichangia na kuviwezesha vyombo vya kanisa.
Hayo yamesemwa na Padre Adeodatus Rwehumbiza Paroko wa Parokia ya Bukoba, katika kilele cha hija ya Bikira Maria wa Lurdi, Nyakijoga Parokiani Mugana , Misa iliyoongozwa na Askofu Methodius Kilaini Jimboni Bukoba.
Katika homilia yake Padre Adeodatus amewasihi waamini kutegemea maombezi yenye nguvu ya mama yetu Bikira Maria hasa kwa kusali Rozari takatifu ambapo hutusaidia kuepukana na majanga na uonevu wa mwovu shetani na kusema kuwa ni vema wakristu kujiweka karibu na mama mwenye huruma kwa kujiunga na vyama vya kitume vyenye karama ya Bikira Maria jambo litakalo saidia kukua kiimani na kutafuta utakatifu
Aidha ameongeza kwa kuwataka waamini kupenda kuchangia utume wa Radio Maria ili kusaidia kufikisha habari njema ya Yesu kristu kote duniani,na amehitimisha kwa kuwaomba waamini kujenga tabia ya kutembelea kituo cha hija Nyakijoga na kujitoa kukitegemeza kwani hija ni safari ya imani kutafuta neema ya Mungu na kwa Nyakijoga hija hueleza ukuu wa Maria
Kwaupande wake Askofu msaidizi Jimbo katoliki Bukoba Methodius Kilaini amezitaka familia kuishi vyema katika misingi ya sala na wakina mama kufuata nyayo za mama Maria na kuwalea watoto vema huku nao watoto wakitakiwa kuishi kwa upendo,sanjari na vijana kuutumia ujana wao vizuri ili baadae wafaidi matunda ya ujana wao.
Katika Misa hiyo Askofu Rwoma alizindua Sinodi ya Maaskofu Jimboni Bukoba Pamoja na Jubilei ya Miaka 50 ya Utume wa WAWATA Kitaifa kwa ngazi ya jimbo pamoja na Jubilei ya Miaka 50 ua utume wa Askofu Kilaini na Padre Kalikawe